MATANDALA

Tuesday, July 24, 2012

What is industrial engineering and management?


"Industrial engineering and management is concerned with the design, improvement, installation and management of integrated systems of people, materials, information, equipment and energy. It draws upon specialized knowledge and skills in the mathematical, physical and social sciences, together with the principles and methods of engineering analysis and design, to specify, predict, and evaluate the results to be obtained from such systems."
http://www.udiemso.udsm.ac.tz/?page=Downloads

Wednesday, June 6, 2012

Ubuyu una kinga kubwa ya mwili!!!!!!

Inaaminika na baadhi ya watu kuwa ubuyu ni tunda lisilokuwa na thamani sana, kwani hata mtu akiwa anafanya biashara ya kuuza ubuyu hudharaulika, pengine ni kutokana na watoto na watu wa hali ya chini kupenda kutumia. Lakini habari za hivi karibuni zinatoa taswira tofauti kuhusu tunda hili. Taswira hii inaweza kabisa kubadilisha mtazamo wa baadhi ya watu waliokua wakilidharau tunda hili. Hivi karibuni Jumuiya ya Ulaya (EU) imeidhinisha kuingizwa kwa tunda hili barani humo kama tunda la kibiashara baada ya kampuni ya PhytoTrade Africa kupewa kibali cha kuingiza tunda hilo kutoka Afrika. Kampuni hiyo hivi sasa imeruhusiwa kuingiza ubuyu katika bara hilo na kutumiwa na wananchi wake kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuchanganya na vyakula mbalimbali vya nafaka ili kuongeza virutubisho. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, Ubuyu una kiwango kikubwa cha Vitamin C kuliko chungwa. Imegundulika kuwa kiasi cha gramu 100 ya ubuyu ina miligramu 300 za vitamin C, kiasi ambacho ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye tunda kama chungwa ambalo ndilo linaaminika kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin hiyo. Kama inavyojulikana, Vitamini C ni muhimu sana mwilini kwani ndiyo inayotukinga dhidi ya magonjwa nyemelezi mbalimbali yanayoweza kutupata pale mwili unapokuwa hauna kinga ya kutosha, ndiyo maana hata hapa nchini imekuwa ikisisitizwa na wataalamu wetu wa lishe kuwa wagonjwa wenye upungufu wa kinga mwilini au wenye virusi vinavyosababisha Ukimwi, wapende kutumia ubuyu ili kuongeza kinga zao. Hii inatokana na ukweli kwamba ubuyu una virutubisho vingi vya kulinda mwili. Inaelezwa pia na watafiti kuwa ubuyu una vitamini muhimu inayojulikana kama Vitamini B2 ambayo huimarisha ukuwaji wa nyama, ngozi na wa nuru ya macho. Halikadhalika kuna vitamini B3 ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mchakato wa umeng’enyaji wa chakula mwilini. Mbali ya vitamini, ubuyu pia una madini na mafuta aina ya ‘fatty acids’. Gramu 100 za ubuyu ina kiasi cha miligramu 293 za madini aina ya kashiamu, miligramu 2.31 za potasiamu na miligramu hadi 118 za fosforasi (phosphorus). Hivyo utaona ubuyu ni muhimu kiasi gani kwa mwili wa binadamu kutokana na kusheheni vitamini na madini hayo kwa wingi. Aidha, ubuyu unatibu pia ugonjwa wa kuharisha kama vile ambavyo umekuwa ukitumiwa enzi na enzi na mababu zetu walipokutwa na tatizo la Kipindupindu au mfumko wa magonjwa ya kuharisha na kutapika. Kwa mujibu wa habari za hivi karibuni, biashara ya ubuyu inatarajiwa kuongezeka barani Afrika, hasa nchini au mikoa inayolima tunda hili kwa wingi, kama vile Mkoa wa Dodoma na mingine.

Sunday, May 8, 2011

USIOMBE IKUKUTE UMESIMAMA KWENYE DALADALA

MTAANI KWETU


NI mitaa ya Mabibo hostel ambako wasomi wengi wanaishi ila mvua kidogo mitaro inajaa,,,

Saturday, April 23, 2011

UNANIJUA UNANISIKIA?????


Mwana FA a.k.a James Bond

FACEBOOK NOMAAAAAAAAAA


Kweli facebook ni nomaaa

FID Q KUACHIA KITABU (SWAHILI KID) MWEZI AUGUST


Fareed kubanda anategemea kuachia kitabu ambacho amekipa jina la Swahili Kid (mtoto wa kiswahili) ikifika mwezi wa nane ambapo atakuwa akielezea na kushare experience yake kwenye game nzima ya muziki, tangu alipoanza mpka hivi sasa alipofikia.