MATANDALA
Friday, April 16, 2010
NAKAYA DECLARED HER CHOICE ON POLITICAL PART
Hey people, its been a min since i posted something fresh. i have just been swamped with all kinds of activities. In short, i have been on the hustle.
Over the weekend niliwaita waandishi wa vyombo vya habari mbali mbali. Nia yangu ya kuwaita ni kuwatangazia watanzania wenzangu kuwa nimejiunga rasmi na chama cha demokrasia na maendeleo (chadema)
Uamuzi wangu umefuatia muda mrefu wa kuangalia vyama vyetu tofauti tofauti na i decided that chadema was best for me. Ni chama cha vijana shupavu na jasiri. wana ndoto zinazoendana na za kwango. Most of all, they have real passion. Something i have not seen in other parties.
I have realized i need to start practicing what i preach. One very wise man said 'BE THE CHANGE YOU WANT TO SEE' Haileti maana kabisa sisi kama watanzania waliopevuka kunyamaza au kutofanya chochote kuhusu haya matatizo tunayoyapitia. Je, wewe unaona sawa wanawake wajawazito kujifungulia chini? unaona sawa wagonjwa kushare vitanda? Unaona ni haki kupewa maji au umeme watapojiskia sababu ya wananunua mashine feki?
Kwa kweli nimechoka kufanywa mpumbavu.Wewe je? Haiwezekali Tanzania ikawa na rasilimali nyingi kiasi hichi na bado watu wanasota hivi jamani!Eti katika nchi masikini duniani, na sisi tupo!! Wanaokaa arusha, jaribu kupitia pale mount meru hsp ujionee maajabu. au wa moshi, katiza pale KCMC emergency room uone Tanzania tunakoelekea. Pia pitia wodi za akina mama uone dharau wanawake tunaopewa. Have you forgotten kwamba WE ARE THE BACKBONE OF THIS NATION? Tupo sehemu ya kusikitisha sana. Its time to RISE!
Ni aibu kwetu sisi kufumba masikio, na kusema hatutahusika na siasa. hatuta piga kura wala kuwa na chama. AMKENI!!! Enyi vijana, huu ndio muda wa kufuta wizi wa mali zetu. Sisi sio masikini. Sisi ni matajiri. Na mkicheza tena mwaka huu, mtapewa dozi kali kuliko iliyotokea hii miaka mitano chama tawala iliyotupa. Nyerere once described Tanzania as a country "stinking with corruption."
"Corruption in Tanzania has no bounds. Every country I visit they talk about corruption in Tanzania. Tanzania is stinking with corruption," Nyerere told journalists gathered at the Tanzania Press Club.
Referring to a tax fraud in the country that recently led to aid suspension by donor countries and organizations, Nyerere declared: "This was one quality of corruption."
"Any government that works for the wealthy does not collect tax, it chooses to harass small-time dealers," Nyerere charged. Je hamuoni haya mambo yanayofanywa na chama cha mafisadi yalishatabiriwa na Baba wa Taifa? Hicho chama sio cha mwananchi wa kawaida ndugu zangu, ni cha walionazo na wanaotaka kuzidi kutumaliza. Tunachohitaji, watanzania wenzangu, vijana wenzangu na wanawake wenzangu ni MATUMAINI na HAKI. Tumekuwa tukikatishwa tamaa kwa muda mrefu sana.Naona mwanga- CHADEMA. Napenda kuwahisi na nyie kujiunga na hichi chama chenye mwelekeo. Hebu tupiganie mabadiliko yetu wenyewe ndugu zangu. Tuchukue hatua kwa namna yoyote ile, tupate haki zetu.
Tukiuliza maswali sahihi, na kwa nia thabiti nina imani tutapata majibu tunayostahili na sio kuyeyushwa tunavyoyeyushwa.
Kuwa mabadiliko unayotaka kuyaona.
The harder the battle, the sweeter the victory!
I AM THE DAUGHTER OF NYERERE! And if he was alive today- trust me...angekuwa CHADEMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment